Ep. 10 - Salama Na MwanaFA | KARAMA

Salama Na

02-04-2020 • 55 mins

Weekend mbili zilitopita rafiki yangu Mwinyi aka Mpwa aka Cousin aka Hamis alikua akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake na alikua amefiksha umri wa kustahili kusherehekea kwa kweli na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha, mke wake kipenzi alinipigia simu siku nne kabla ya birthday ya mumewe na kutaka tujumuike nae kum suprise, pia akaniambia ana kazi sana ya kuweza kukamilisha hilo tukio maana jamaa (Mwana FA) kashasema yeye hana mango wa kutaka shughuli, angependa maisha yaendelee tu kama kawaida. Pengine alikua akitarajia dinner nyumbani na mkewe na wanawe basi. So kukawa na zoezi hapo la kuhakikisha jamaa hasomi mchongo na kwamba zoezi ni lazima lifanikiwe. Malika binti yeke kwa kwanza ndo alikua amiri jeshi mkuu wa kuhakikisha Baba anarudi nyumbani by saa mbili usiku ili ale na familia chakula cha usiku. Suala hili lilizidi kuwa tamu pale Malika alipofanikiwa kutimiza ombi lake kwa Baba na sisi wengine ikawa rahisi kuibuka nyumbani na kumaliza mchongo mzima. Ulikua usiku mzuri ambao umeandaliwa kwa mapenzi mengi, na kila kitu kilipangwa kwa uangalifu by saa nne unusu tunaimba kata keki tule 😃. Ila kitu unique kabisa kwenye sherehe hiyo ilikua ni vipande vya karatasi ambayo tuligaiwa, vilikua na namba na namba yako ikitajwa basi kuna swali ilikua unatakiwa kulijibu, ili kuonyesha ukaribu wetu, unataka kujua mimi nilipata swali gani? Ok, swali lilikua ni kama nakumbuka siku yangu ya kwanza kukutana na Mwana FA!    Hiyo story itaendelea siku nyengine ila kwa sasa nikuambie tu mahusiano yangu na yeye Mwinyi. Tumekua pamoja naweza sema baada ya kukutana hapa mini Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 2000, sote tukiwa wembamba na watoto tu, ila bila ya shaka kila maja akiwa na nia na madhumuni ya kufika hapa tulipo na zaidi panapo majaaliwa, kuna smile flani ivi ambalo mpaka leo halijawahi kubadilika ndo ID yake pamoja na mwanya flani unaokamilisha muonekano wake, style za misuko ya nywele tofauti pia ilikua ikimtenganisha yeye na wanamuziki wengine, ila kikubwa zaidi ambacho kinamfanya yeye awe kasimama mbali na wenzake ni jinsi anavyoandika, anavyowasilisha na anavyowakuna pia washabiki wake ambao kila siku zinavyozidi kwenda wamekua wakiongezeka, nadhani ni baada ya kampa sikio la moja kwa moja ambako kumewafanya wamsikilize kwa umakini zaidi.    Siku za hivi karibuni rafiki yangu aliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii zaidi Twitter baada ya kuamua kujiita yeye Shaaban Robert wa enzi zetu, kama ulikua hufahamu Shaaban Bin Robert alikua mi mshairi, muandishi wa vitabu na essay na pia inaaminika alikua moja kati ya wafikiri wazuri wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika ya Mashariki. Mwana FA ni mmoja kati wa washairi wazuri na mwenye style tamu pia ya kuwakilisha uandishi wake kwa miaka mingi sasa ya muziki huu wa kizazi kipya. Kama unadhani anastahili kujiweka ligi moja au hata nyumba moja na Shaaban Robert au pengine hana nafasi hiyo mimi sina cha kusema juu ya hilo, ila ninaloweza kusema ni kwamba rafiki yangu huyu ameonekana kukua mbele ya macho yangu kwa zaidi ya miaka kumi na tano sana, alianza kufanya kazi zake mapema tu kama solo artist na ngoma sake ya kwana tu ilikua HIT, Unaikumbuka INGEKUA VIPI? Kisha ikaja ECT, baadae kama Duo yeye na AY huku akiwa anaendelea kufanya solo projects na baada ya hapo ameendelea kusimama mwenyewe na kujiimarisha kila mara anapotupa nyimbo mpya, na kwa hilo basi niko hapa kwaajili ya kutoa heshima zangu kwake na kumtakia kila lenye kheri naye.    P.S  Mwana FA pia ni rafiki mzuri na Baba kipenzi kwa mabinti zake.    Enjoy.  Love,  Salama.  Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ  Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

You Might Like

The Rest Is Politics
The Rest Is Politics
Goalhanger Podcasts
Leading
Leading
Goalhanger Podcasts
Newscast
Newscast
BBC News
Ukraine: The Latest
Ukraine: The Latest
The Telegraph
Today in Focus
Today in Focus
The Guardian
FT News Briefing
FT News Briefing
Financial Times
Political Currency
Political Currency
Persephonica
Page 94: The Private Eye Podcast
Page 94: The Private Eye Podcast
Page 94: The Private Eye Podcast
The Teacher's Pet
The Teacher's Pet
The Australian
The Daily
The Daily
The New York Times
Tortoise Investigates
Tortoise Investigates
Tortoise Media
The Trawl
The Trawl
Jemma Forte & Marina Purkiss
Economist Podcasts
Economist Podcasts
The Economist